P SQUARE MAHAKAMANI KWA KUVUNJA MKATABA
Posted by
Unknown
| Monday, September 10, 2012 at 5:53 AM
0
comments
Labels :
May D ndio msanii kutoka Nigeria aliye fanya vizuri zaidi kwenye wimbo wa P Square ,Chop My Money walio mshirikisha Akon kutoka Marekani . Msanii huyu alikuwa chini ya Square Records na North Side Entertainment limited. Mkataba wake ulisitishwa na lebel hizi mbili katikati ya mwezi wa 8 , 2012 bila yeye kupewa taarifa na alipata habari za mkataba wake kusitishwa kupitia vyombo vya habari kama blogs ,websites na radio station zilizo mpigia simu kutaka kujua sababu ya yeye kupigwa chini Square Records baada ya kufanya kazi nzuri na P Square kwenye chop my money. Sababu iliyotolewa na msemaji wa lebel hizo ilikuwa kutofautiana maamuzi na ufanyaji wa kazi . Baada ya kufahamu yote hayo May D amefungua kesi akidai P Square wamevunja mkataba kiholela bila kumpa taarifa kamili kama walivyo fanya awali wakati wanaingia mkataba na record lebel yao .Fahamu kuwa kaka mkubwa wa P Square Jude Okoye ndiye aliye toa taarifa hizo kama ilivyo andikwa hapo chini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)