Follow us on:

Pages

DANNY MRWANDA AVUTA JIKO

Zilikua nderemo na vifijo pale tofauti za kiitikadi katika mchezo wa soka la Bongo -za U-Simba na U-Yanga, zilipowekwa kando na kuwezesha tukio la kihistoria kuandikwa wakati kijana mtanashati wa haja kabisaaa, superstar wa ukweli, mchezaji wa kimataifa na timu ya taifa (Taifa Stars), Danny Mrwanda alipotamka maneno mataaaam 'Yes I do' kwake Mrembo mwenye tabasam la asili na ucheshi wa kutokukera, Bi Lucy Dule pale katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)-Kimara-Bonyokwa na kua rasmi MR & MRS DANNY D. MRWANDA. Uhondo huo haukuishia hapo, ulisonga katika ukumbi maarufu jiji la D'salaam pale Sinza kwa wajanja, Deluxe...full kiyoyooooo. Huwezi kuamini! Mpambe wake ni mpinzani wake katika soka...SHADRACK NSAJIGWA na mkewe JANE SHADRACK NSAJIGWA. Kitu cha kufurahisha, wale wasimamizi wa karibu (maids & groom's men) walikua ni marafiki zake katika soka kutoka Simba na Yanga wakiongozwa na Uhuru Selemani (Simba) na Nizar Khalfan (Yanga) wakiwa na wake zao. Hapa utapata uhondo wa shughuli ya Deluxe iliyo pachikwa jina rasmi THE MRWANDAS' NIGHT.... Colours; Red, Gold, White, Black, Tangerine Tango!! TIRIRIIIIIKA!