MAZUNGUMZO BAADA YA KUKUTANA NA MAU (JOHNSON) WA THE MAHOKA'Z
Posted by
Unknown
| Thursday, September 27, 2012 at 12:55 AM
0
comments
Labels :
Nilikutana na Mau ambae ni mchekeshaji wa muda mrefu ambae pia amepata nafasi ya kuonekana katia katika baadhi ya video za Bongo fleva akiigiza, Haya ndio mazungumzo yetu baada ya kukutana nae. AN : mambo vp kaka?
Mau: shwari tu mwanangu mwenyewe,
AN: kunakitu kinasumbua masikio yangu, yaan nakisikia sana kinaitwa The Mahoka’z hii ikoje kaka, na nini maana yake?
Mau :mahokazi ni vichekesho bila kufata script, sasa sisi tunavibadilisha na kuwa vichekesho vya kufata script,pia ni comedy safi tofauti na zingine ambazo unaziona hapa bongo.
AN: idea ilikua ni nini mpaka mkatengeneza hiki kitu?
Mau : mimi nilikutana na kiongozi wa kampuni ya EML ambae ni mshikaji wangu sana, akaniambia nikikupa air time utafanya nini?,nikamwambia naweza kufanya kipindi kizuri tu,akasema mimi nataka kiwe cha komedi,nikamwabia sasa mimi ntafanya kipindi gani tofauti na komedi wakati ndio nyumbani kwangu humo,nikawatafuta washikaji ambae ni Ringo na Tiny white tukaka nakufikiria cha kufanya tukaona tufanye kitu tofauti na wengine ndio idea ikaja ya kufanya komedi katika jumba,
AN : je tutarajie kuona watu wengine tofauti na joh, john na Johnson?
Mau :yaah utaona watu tofauti wakiingia na kutoka,wasanii wakubwa wataonekana comedian wengine pia utawaona ,kwasababu katika jumba hilo yatakua ni maisha ya kawaida sasa siku tukiwa tunajifunza kuimba utamuona msanii kabisa kaja kutufundisha kuimba,siku tunajifunza kuigiza atakuja muigizaji kutufundisha.
AN: kwanini mmejiita majina yanayofanana?
Mau: sisi ni watoto wa mama mmoja ila baba tofauti kila mtoto ana baba yake na karithi tabia kutoka kwa baba yake,kwahiyo mama akatupa majina hayo ili tusipotee.
AN: watoto wa mama mmoja baba tofauti inakuaje hapo?
Mau : yani watanzania wajiandae kucheka kwa hiari yao bila kulazimishwa,kwa sasababu kutakua na vituko sana kila mmoja anaakili zake alizo rithi kwa Baba yake .
AN: tutarajie nini kipya kutoka kwenu Mau Yule tulio mzoea ,Ringo pamoja na Tiny White..?
Mau: hapa mtarajie kumuona joh john na Johnson kwa sababu tumebadilika kabisa sisi hatukopy na kupest kama wengine ,ukiangalia komedi nyingi ni za habari habari tu sasa sisi tuko tofauti kabisaaa.
AN: je mko chini ya uongozi wowote au mnajiongoza wenyewe tu?
Mau: sisi tuko chini ya uongozi wa EML,ndio watasimamia kazi zote katika The Mahoka’z.
AN: nani kiongozi au msemaji wa The Mahoka’z?
Mau: Mimi ndiyo msemaji na kiongozi huoni ninavyo jishebedua kuongea.
AN: tupe neno lolote la mwisho..
Mau: Mahoka’z iko njiani wiki ijayo tunaanza kazi na baada ya wiki tatu tarajia kutuona kwenye TV yako ,komedi safi yaani “world class comedy” kukuchekesha kwa hiari yako bila kulazimishwa.
AN: aksante kwa muda wako kaka..
Mau: poa poa mwanangu mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)