NISHA NAE APATA PEDESHEEE NA LAMNUNULIA GARI LA THAMANI
Posted by
Unknown
| Monday, August 20, 2012 at 3:34 AM
0
comments
Labels :
Mwana-filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kununuliwa gari na jamaa flani ambaye anatajwa kwamba ni pedeshee wa nguvu.
Nisha, anadaiwa kununuliwa gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser Prado lenye namba za usajili T 765 BBT.
MFANO WA GALI ALILONUNULIWA NISHA
Chanzo makini kimesema, Nisha amempata pedeshee wa nguvu ambaye ni mtumishi mwenye ngazi kubwa serikalini.
“Unajua Nisha hataki kumuweka wazi huyo kigogo kwa sababu kwanza ni mume wa mtu, pia ni mtu anayefanya kazi serikalini hivyo kwa kukwepa hilo anadai gari hilo amelinunua jambo ambalo si kweli, ingekuwa sanaa inalipa hivyo, basi wasanii wote wa filamu wangekuwa na magari,” kilisema chanzo hicho.
Nisha alipoulizwa, aliruka kimanga kununuliwa mchuma huo na pedeshee wa nguvu, isipokuwa akadai kununua ndinga hilo kwa fedha zake mwenyewe.
“Jamani jamani! Hili gari nimelinunua kwa pesa zangu na nimezipata kutokana na filamu ninazouza, nawashangaa mnaponiambia nimehongwa, nimelinunua kwa shilingi milioni 60.
“Wasanii wengi wanasema filamu hazilipi lakini kwangu zinalipa kwani nimepata mafanikio mengi ambayo sikuyategemea, wanaosema hazilipi ni wale wanaoshirikishwa kwenye filamu lakini mimi nacheza za kwangu,” Nisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)