Follow us on:

Pages

JUMA NATURE KUACHIA NGOMA MBILI KWA MPIGO

Juma Nature afyatua mawe mawili Mwana Bongo Fleva, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, ameonesha mwaka huu hataki utani, kwani ameachia mawe mawili kwa mkupuo. Nature, ameachia ngoma hizo, ya kwanza ikiitwa Kijijini na nyingine ameipa jina la Usicheze Peke Yako. Kwa muda mrefu sasa, Nature amekuwa akifanya shoo kwa kutumia nyimbo zake za longtime pasipo kutoa hit mpya. Tathmini imeonesha kuwa nyimbo hizo mpya, zitamrudisha sawia, kwani zina ubora unaokubalika. Kijijini, Nature ameimba kwa kumshirikisha mrembo wa Bongo Fleva, Baby Madaha, wakati Usicheze Peke Yako, ameufanya na memba wenzake katika Kundi la TMK Wanaume Halisi.