Follow us on:

Pages

J Dee Barnaba watumbuiza katika hafla fupi ya uzinduzi wa huduma za ndege wa QATAR AIRWAYS kutoka KIA.

Lady Jay Dee akiimba kwa msisitizo kabisa mbele ya wageni (hawapo pichani) waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana sana,ambayo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali katika Hoteli ya Mount Meru jiji Arusha wakati wa hafla fupi ya kusherekea kwa uzinduzi wa Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118
Mmoja wa wasanii mahiri kutoka kituo cha wenye vipaji cha THT,Barnabas sambamba na bendi yake kwa pamoja wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi rasmi wa kusherekea kwa uzinduzi wa Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.Tafrija hiyo ilifunguliwa rasmi na mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe.
Barnaba akiimba huku akipiga kitaa kuonesha kipaji chake alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana sana,ambayo ilihudhuria na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali.