Hii ndiyo aibu ya Miss wa Lundenga
Posted by
Unknown
| Saturday, August 25, 2012 at 2:46 AM
0
comments
Labels :
Mrembo aliyeshiriki Miss Tanzania mwaka jana, Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania kufuatia kwenda kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012 nchini Nigeria hivi karibuni wakati hasomi chuo chochote. Ukweli upo hivi, ili mrembo ashiriki shindano hilo, linalopokea walimbwende kutoka barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo vya nchini mwake sifa ambayo Hamisa hakuwa nayo. Ripota wetu alimtafuta Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo hasa ikizingatiwa kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa Jensen aliibuka kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili. “Ni kweli Hamisa ni miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria kushiriki shindano hilo sifahamu aliutoa wapi? Najua hakuna chuo chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna mashindano kama hayo kwangu,” alisema Lundenga. Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini. Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua. “Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top ten, lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho (pichani chini), lakini siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)